Matthew 11

Isa Na Yahya Mbatizaji

(Luka 7:18-35)

1 aBaada ya Isa kumaliza kutoa maagizo kwa wanafunzi wake kumi na wawili, aliondoka hapo akaenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao.

2 bYahya aliposikia akiwa gerezani mambo ambayo Al-Masihi
Al-Masihi maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
alikuwa akiyafanya, aliwatuma wanafunzi wake
3 dili wakamuulize, “Wewe ndiye yule aliyekuwa aje, au tumngojee mwingine?”

4Isa akajibu, “Rudini mkamwambie Yahya yale mnayosikia na kuyaona: 5 eVipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema. 6 fAmebarikiwa mtu yule asiyechukizwa na mimi.”

7 gWale wanafunzi wa Yahya walipokuwa wanaondoka, Isa akaanza kusema na makutano kuhusu Yahya Mbatizaji. Akawauliza, “Mlipokwenda kule nyikani, mlikwenda kuona nini? Je, ni unyasi ukipeperushwa na upepo? 8Kama sivyo, mlikwenda kuona nini basi? Mtu aliyevaa mavazi ya kifahari? La hasha, watu wanaovaa mavazi ya kifahari wako katika majumba ya wafalme. 9 hBasi mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumwona nabii? Naam, nawaambia, yeye ni zaidi ya nabii. 10 iHuyu ndiye ambaye habari zake zimeandikwa: “ ‘Tazama nitamtuma mjumbe wangu mbele yako,
atakayetengeneza njia mbele yako.’

11 jAmin, nawaambia, miongoni mwa wale waliozaliwa na wanawake, hajatokea mtu aliye mkuu kuliko Yahya Mbatizaji. Lakini aliye mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni ni mkuu kuliko Yahya. 12 kTangu siku za Yahya Mbatizaji hadi sasa, Ufalme wa Mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wanauteka. 13 lKwa maana manabii wote na Torati walitabiri mpaka wakati wa Yahya. 14 mIkiwa mko tayari kukubali hilo, yeye (Yahya) ndiye yule Ilya ambaye manabii walikuwa wamesema angekuja. 15 nYeye aliye na masikio, na asikie.

16 o“Lakini kizazi hiki nikifananishe na nini? Kinafanana na watoto waliokaa sokoni wakiwaita wenzao na kuwaambia,
17 p“ ‘Tuliwapigia filimbi,
lakini hamkucheza;
tuliwaimbia nyimbo za maombolezo,
lakini hamkuomboleza.’

18 qKwa maana Yahya Mbatizaji alikuja, alikuwa hali wala hanywi, nao wanasema, ‘Yeye ana pepo mchafu.’ 19 rMwana wa Adamu alikuja akila na kunywa, nao wanasema, ‘Tazameni huyu mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na “wenye dhambi.” ’ Lakini hekima huthibitishwa kuwa kweli kwa matendo yake.”

Onyo Kwa Miji Isiyotubu

(Luka 10:13-15)

20 sNdipo Isa akaanza kushutumu miji ambamo alifanya miujiza yake mingi kuliko kwingine, kwa maana watu wake hawakutubu. 21 t“Ole wako, Korazini! Ole wako Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu, ingefanyika Tiro na Sidoni, miji hiyo ingekuwa imetubu zamani kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu. 22 uLakini nawaambia, itakuwa rahisi zaidi kwa Tiro na Sidoni kustahimili katika siku ya hukumu, kuliko ninyi. 23 vNawe Kapernaumu, je, utainuliwa hadi mbinguni? La hasha, utashushwa mpaka kuzimu.
Kuzimu ni Mahali pa wafu.
Miujiza iliyofanyika kwako ingefanyika huko Sodoma, mji huo ungalikuwepo hadi leo.
24 xLakini nakuambia kwamba, itakuwa rahisi zaidi kwa Sodoma kustahimili katika siku ya hukumu kuliko wewe.”

Hakuna Amjuaye Baba Ila Mwana

(Luka 10:21-22)

25 yWakati huo Isa alisema, “Nakuhimidi Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, nawe ukawafunulia watoto wadogo. 26Naam, Baba, kwa kuwa hivyo ndivyo ilivyokupendeza.

27 z“Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu: Hakuna mtu amjuaye Mwana ila Baba, wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana na yeyote ambaye Mwana anapenda kumfunulia.

Isa Awaita Waliolemewa Na Mizigo

28 aa“Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 abJifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. 30 acKwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.”
Copyright information for SwhKC